header image

Afya ya kiakili

Nitapata wapi msaada?

mental help2

Hakuna haja ya kuwa na aibu ikiwa unasumbuliwa na suala la afya ya akili. Ni jambo ambalo wanaume wengi wanasumbuliwa, hata kama hawazungumzii juu ya hili.

Unaweza kuanza kwa kuzungumza na marafiki au wapendwa wako kupata msaada. Wajulishe kwamba hujisikii vizuri.

Ikiwa hujisikii kama unaweza kuzungumza na marafiki au hata kama unatazungumza nao, unapaswa kuzungumza na muuguzi au mhudumu wa afya kwenye zahanati  karibu yako. Baadhi ya maswala ya afya ya akili yanahitaji ushauri au hata dawa.

Unaweza pia kuangalia baadhi ya mashirika ya mitaa karibu yako ambayo yanaweza kukupa maelekezo ya huduma.

Hatua ya kwanza ni kuomba msaada, tambua kuwa haujisikii vizuri.