Kuna hatua nyingi rahisi tunazoweza kuchukua zote kuzuia VVU.
Hatua hizi zinafanya kazi bora zaidi pamoja. Kwa hiyo, ikiwa moja inashindwa au tunasahau kuitumia, basi tunaweza bado kutegemea nyingine ili kutusaidia kuishi bila VVU.
Walio na VVU kati yetu wanaweza pia kuchukua hatua za kuhakikisha hatuambukizi VVU kwa wengine.
Kutumia kinga na kinga inayoambatana wakati wa kufanya ngono
Kutumia kinga ni ulinzi madhubuti dhidi ya VVU na magonjwa mengine ya ngono kwa sababu huzuia kubadilishana kwa maji ya mwili ambayo yanaweza kuwa na VVU (shahawa na damu).
Wale kati yetu ambao wana VVU wanapaswa pia kutumia kinga wakati tunapofanya ngono ili kusaidia kuzuia kuenea kwa VVU kwa wengine na kutuzuia kupata magonjwa mengine ya ngono. Pata taarifa zaidi kuhusu jinsi ya kutumia kinga hapa.
Je, ulijua kwamba kuna njia sahihi na njia zisizo sahihi za kutumia kondom?
- Usitumie kinga zaidi ya moja kwa wakati mmoja kwenye uume wako. Unaweza kufikiria hii inakufanya uwe salama zaidi. Lakini haifai. Kwa kweli kinga zinaweza kupasuka kutokana na msuguano kati ya kinga hizo
- Ikiwa unapenda ngono na mtu zaidi ya moja basi tumia kinga mpya kila wakati unapoingia kwa mpenzi mpya ili kuepuka kueneza VVU na magonjwa mengine ya ngono
- Pata kinga ambazo zinakufaa kwa vile zinakuja kwa maumbo na ukubwa tofauti. Hapa kuna baadhi ya maeneo ya kupata kinga
- Daima utumie kinga inayotumika na mafuta-maji, hasa kwa ngono ya mkundu. Usitumie mafuta ya mgando au mate. Pata maelezo zaidi chini
Mafuta- maji, ni kitu kinacho sababisha eterezi ambao unafanya kuwa ngono ya mkundu kuwa nzuri zaidi na ya kujifurahisha. Pia inazuia mkundu wako au uume wako kuumia au kuharibiwa kutokana na msuguano.
Mafuta-maji, kama mafuta ya maji, ni bora zaidi ya kutumia kwa kondomu kwa sababu mafuta ya mgando yanaweza kuharibu kinga. Tunapotumia mafuta-maji, tunapaswa kukumbuka:
- Mafuta ya kupikia, mafuta ya mtoto, mafuta ya mgando na mafuta ya ngozi na ya mikono hayapaswi kutumiwa kwa sababu yatapasua kinga yako
- Kutumia mate haisaidii kutereza kwa kutosha kutumiwa kama mafuta-maji kwani hukauka haraka na yanaweza kueneza magonjwa mengine ya ngono (ingawa VVU haipo katika mate)
- Daima weka mafuta-maji mengi zaidi kwenye mdomo wa mkundu na kwenye kinga baada ya kuweka kabla ya kuanza kufanya ngono. Ikiwa ngono huanza kuwa kavu au inanata, tumia zaidi mafuta-maji kulinda kinga na kukuwezesha wewe na mwenzi wako kuwa na furaha
Kutumia dawa za ‘kuongeza maisha’ ili kuzuia VVU
Je, unajua baadhi ya dawa za kuongeza maisha ambazo tunatumia kutibu watu wenye VVU pia zinaweza kutumika kuzuia maambukizi ya VVU?
Kutumia dawa hizi kabla ya kuambukizwa VVU huitwa PrEP (Pre-Exposure Prophylaxis) na kuitumia katika masaa 72 baada ya kukutana na VVU inaitwa PEP (Post Exposure Prophylaxis).
PEP
Labda kinga ilipasuka wakati wa kujamiiana au unafikiri umeambukizwa VVU kwa namna nyingine. Je, utafanya nini? Unaweza kupata PEP kutoka kliniki iliyopo karibu nawe. Kufanya kazi, PEP lazima ianzishwe kabla ya masaa 72 (siku 3) zimepita baada ya kufanya ngono na mwenye VVU.
Vidonge vya PEP vinapaswa kunywewa kila siku kwa mwezi mmoja lakini vinaweza kusababisha madhara fulani kama kichefuchefu au kizunguzungu ambacho kinaweza kufanya vigumu kunywa dawa. Baada ya mwezi mmoja utapima tena VVU ili uhakikishe kuwa bado haujaathiri ka na VVU.
PrEP
Ikiwa unafikiri unaweza kuwa una VVU, unaweza kunywa PrEP ili kutokuwa na VVU, hata kama virusi vya ukimwi vimeingia mwilini mwako.
Utahitaji kutembelea zahanati inayotoa PrEP na kukutana na mtoa huduma ya afya kabla ya kuchukua vidonge vya PrEP.
Wanaume wanapaswa kutumia PrEP kila siku kwa angalau wiki kabla ya dawa kuwalinda kutokupata VVU. Wavulana wanaotumia PrEP watahitaji kuendelea kutumia dawa zao kila siku ili kuzuia VVU. Ni muhimu usikose dawa kila kila siku ikiwa bado unataka kinga ya PrEP.
Ikiwa unakumbuka kunywa dawa yako ya PrEP kila siku, PrEP itakupa kinga kwa 92% -100% ya VVU. Hiyo ni zaidi!
PrEP inaweza kukupa madhara madogo ambayo kawaida hupotea.
PrEP sio kinga dhidi ya magonjwa mengine ya ngono. Kutumia PrEP na kinga pamoja ni bora kwa sababu kinga pia hukukinga kwa magonjwa mengine ya ngono.
Unapotaka kutumia PrEP, kumbuka:
- PrEP ni njia bora ya kulinda dhidi ya maambukizi ya VVU hasa kwa wale ambao wanaona vigumu kutumia njia mingine ya kuzuia
- Unapaswa kutumia PrEP kila siku ili ifanyie kazi. Ikiwa hutumii dawa yako ya PrEP kila siku, basi inaweza kushindwa kukulinda kutopata VVU
- PrEP ni imethibitishwa kisayansi kuzuia VVU na kuungwa mkono na mashirika mengi ya matibabu na serikali duniani kote
- PrEP ni salama. Watu tisa kati ya watu kumi ambao hutumia PrEP hawatakuwa na madhara yoyote. Ikiwa utapata madhara yatakuwa madogo na kupotea haraka. Daktari wako atakuwa pia atakufuatilia kama kuna madhara yoyote makubwa na kusitisha matumizi ya PrEP kama ni lazima
- Hautakiwi kutumia PrEP kwa maisha yako yote. PrEP sio matibabu ya VVU ingawa inatumia baadhi ya dawa sawa. Unaweza kuchukua PrEP kwa muda wa maisha yako wakati unadhani unahitaji na kisha kuacha wakati hauko kenye hatari ya maambukizi ya VVU
- PrEP sio kinga dhidi ya magonjwa mengine ya ngono kwa hiyo inapaswa bado kutumika pamoja na kinga na kupima mara kwa mara
- Ingawa PrEP inafanya kazi kwa ufanisi haipatikani kila mahali bado. Angalia orodha yetu ya watoa huduma kwa maelezo Zaidi
Kubadilisha tabia yako
Ukweli ni kwamba, kubadilisha tabia zetu ni vigumu sana, hasa linapokuja suala la ngono. Hata kama wewe si mkamilifu, kama wengi wetu, hapa kuna baadhi ya mambo unayoweza kufanya ili kupunguza hatari ya kuwa na VVU:
- Uchukue kinga na kichupa cha mafuta-maji wakati unapotoka. Utakuwa na uwezekano mkubwa wa kuitumia ukiwa navyo (pata kinga na mafuta-maji hapa).
- Ikiwa hutumii kinga wakati wa kufanya ngono, jaribu kupunguza idadi ya watu ambao unafanya nao ngono bila kinga. Hii sio kamili lakini itapunguza uwezekano ikiwa wewe na washirika wako hupima mara kwa mara. Pata maelezo zaidi juu ya kupima hapa!
- Jihadharini na dalili za magonjwa ya ngono. Unapaswa kujua dalili za magonjwa ya ngono bila kujali idadi ya washirika ulionao. Unaweza kuepuka kufanya ngono na mtu kama unapoona dalili inayoonekana ya magonjwa ya ngono.Kama unapoona dalili kwako mwenyewe, unapaswa kuacha kufanya ngono mpaka uende kupimwa na kutibiwa. Kuwa na magonjwa ya ngono itaongeza hatari yako ya kupata VVU na magonjwa mengine ya ngono. Kumbuka baadhi ya magonjwa ya zinaa hayaonyeshi dalili, hivyo pima mara kwa mara.
- Kunywa pombe kidogo hupunguza hatari kwa sababu kunywa pombe kunaweza kusababisha kukufanya uamuzi mbaya, ni nani unayejamiiana na jinsi unavyofanya ngono.
- Ikiwa unatumia dawa za sindano na sindano hakikisha kutumia sindano na vifaa safi. Pata kila kitu unachohitaji kujua hapa