header image

Afya ya kiakili

Wasiwasi na Huzuni

depression

Wasiwasi

Wasiwasi ni hisia inayohusiana na hofu. Kila mmoja atasikia wasiwasi wakati fulani katika maisha yao. Wasiwasi unaweza kuwa suala la afya ya akili wakati hutokea mara nyingi au unapohisi kama una hali hiyo wakati wote.

Aina hii ya wasiwasi inaweza kuwa na dalili za kimwili na za akili ikiwa ni pamoja na:

  • Kimwili: shida kupumua, kubanwa katika kifua chako, kutokwa jasho sana, mabadiliko ya moyo wako kudunda, kizunguzungu, kichefuchefu, kuhara.
  • Akili: hisia kali ya hofu, kusikia vibaya sana, na wasiwasi mwingi zaidi kuliko kawaida

Aina hii ya wasiwasi inaweza kusababisha sababu nyingi. Kutumia vilevi, kama cocaine au vilevi vingine, inaweza kuongeza wasiwasi. Wanaume wengine wanaojamiiana na wanaume, wanaweza  kuwa waathirika wa unyanyasaji au ubaguzi ambao husababisha hofu na inaweza kusababisha wasiwasi.

Kuelewa wasiwasi ni muhimu kwa sababu inaweza kushawishi jinsi unavyofanya na mambo unayofanya. Wanaume wengine wanaweza kunywa pombe zaidi ili kujaribu na kukabiliana na dalili za wasiwasi na hii inaweza pia kuongeza tabia za hatari kama kufanya ngono bila kinga.

Huzuni

Kila mtu huwa na huzuni  wakati mwingine, hiyo ni sehemu ya kawaida na ya afya kama mwanadamu. Unapokuwa unahuzunika na hali hiyo haishi au huanza kuathiri uwezo wako wa kuishi maisha yako ya kawaida basi unaweza kuwa na huzuni. Hizi ni baadhi ya dalili za huzuni:

  • Unahisi huzuni karibu siku nzima na kwa siku zote
  • Unakata tamaa juu ya maisha yako au unahisi kuwa hauna maana
  • Huwezi kufikiri na kufanya kitu kama kawaida yako
  • Haua msisimko kuhusu shughuli ulizokuwa unazipenda au hauna furaha na maisha ya kila siku
  • Unafikiri a sana juu ya kifo au hata kujaribu kujiua. 

Kama ilivyo na wasiwasi, huzuni unaweza kuwa kitu ambacho watu wanazaliwa nacho na wengine huwatokea kutokana na sababu ya mambo katika maisha yao. Huzuni ni wa kawaida kwa wanaume wanaojamiiana na wanaume kwa sababu ya unyanyasaji, unyanyapaa, na ubaguzi ambao wanapata.

Ikiwa unafikiri unasumbuliwa na wasiwasi au huzuni, tafuta jinsi ya kupata msaada hapa.