header image

VVU

Ninaishi vipi na VVU?

Kuishi na VVU

Ukiwa na matokea yanayosema una VVU unaweza kuwa na hasira, kuchanganyikiwa au hofu. Lakini kumbuka kuwa hakuna ulichobadilika. Bado wewe ni mtu yule aliyekuwa jana. Lakini sasa una habari sahihi ili uhakikishe kuwa unaongoza maisha marefu, ya afya na ya kujiridhisha.

Ni sawa kuhisi hofu au kuchanganyikiwa. Ni kawaida kuwa na hisia hizi baada ya kujua kuwa una VVU. Lakini ni muhimu kukumbuka kuwa kutumia vidonge sahihi kila siku vitadhoofisha  VVU katika mwili wako na inamaanisha unaweza kuishi maisha mazuri.

Sasa kwa kuwa una habari sahihi kuhusu hali yako ya VVU unaweza kufanya maamuzi mazuri kuhusu afya yako. Unaweza kuanza na:

  1. Kujifunza jinsi ya VVU vinavyofanya kazi ndani ya mwili wako na jinsi vinavyoathiri mwili wako
  2. Kuelewa chaguo la matibabu yako
  3. Kujenga mfumo wa msaada kwa marafiki au familia

VVU na afya yako

VVU huathiri miili yetu, hasa mfumo wa kinga na uwezo wake wa kutuzuia kupata ugonjwa.

Wauguzi wa afya wanajua jinsi VVU vinavyoathiri mwili wako kwa kutumia vipimo viwili:

  • CD4 hupima nguvu ya mfumo wako wa kinga. Ikiwa kuna VVU nyingi katika mwili wako, kwa kawaida CD4 yako itakuwa chini.
  • Virusi kipimo cha kujua ni kiasi gani cha VVU katika damu yako.

Tunatumia dawa za kuongeza maisha kama tiba ili kuweka mifumo yetu ya kinga ya mwili imara. Kuweka mfumo wa kinga katika miili yetu imara kwa kutumia vidonge vya kuongeza maisha inamaanisha kuwa tutakuwa na afya. Pia ina maana kwamba kiasi cha VVU katika miili yetu kitapungua.

Hii ni muhimu sana, ikiwa unaendelea kutumia dawa zako kila siku, madaktari na wauguzi hawataweza kuona VVU katika mwili wako. Unapokuwa na virusi visivyoweza kuonekana inamaanisha huwezi kueneza VVU kwa wengine.

Unapoishi na VVU, maambukizi ya magonjwa ya ngono kama vile kaswisi, au vidonda vya uzazi inaweza kuwa mbaya sana. Inakuwa vigumu kwa mfumo wako wa kinga ya mwili kutibu. Ni muhimu kujifunza jinsi unavyoweza kuhusu VVU, magonjwa ya ngono na afya ya ngono: sehemu nzuri ya kuanza ni sehemu ya Maambukizi ya Ngono.

Mbali na kuchukua matibabu, kula chakula bora, ikiwa ni pamoja na matunda na mboga, ni muhimu. Kuepuka msongo wa mawazo kwa mwili wako, kama vile kunywa pombe sana, pia ni muhimu. Tunza mwili wako na mwili wako utakutunza. Usisahau, kama  mtu yeyote, wanaume wanaoishi na VVU wanaweza bado kupata baridi au malaria. Ikiwa unasikia mgonjwa sana, badala ya kuwa na wasiwasi, nenda ukamuone muuguzi wa afya.

Kuelewa Matibabu ya VVU

Kumbuka kila wakati, kwa sababu tu una VVU haimaanishi kuwa hauwezi kuwa na maisha mazuri na kuishi hadi kuwa mzee. Sisi sote ambao tuna VVU tunahitaji kukumbuka kutumia vidonge vya kuongeza maisha kila siku na kuzingatia miili yetu.

Tunapotumia dawa za kuongeza maisha virusi hudhibitiwa kwenye miili yetu. Mfumo wetu wa kinga unaweza kufanya kazi zake na kulinda maambukizi mengine kwenye miili yetu (kama vile TB).

Mara unapoanza matibabu ya dawa za kuongeza maisha, utahitaji kuchukua dawa zako kila siku kwa maisha yako yote ili kuzuia ukuaji wa VVU.

Ni wazo baya kuanza kutumia dawa na kuacha kwa sababu hii itatoa nafasi kwa VVU kukua tena ndani ya mwili wako. Ikiwa unaacha kutumia  dawa na kisha kuanza tena, dawa hazitakuwa na nguvu.

Wanaume wengine wana wasiwasi juu ya madhara (madhara hasi) ya dawa za kuongeza maisha, lakini vidonge vya kisasa havina madhara mengi, na zile zenye madhara ni rahisi kuzituliza.

Miongozo ya sasa ya matibabu ya VVU inapendekeza matibabu ya kila mtu aliye na VVU bila kujali kiwango chako cha CD4.

VVU na uhusiano wako

hiv relationWakati gani nitamwambia  mtu nina VVU? Ninawaambiaje?

Haya ni maswali ya kawaida ambayo sisi wote tunayo wakati tunapojua kuwa tuna VVU au wakati mwingine tuliishi na VVU kwa muda fulani.

Jambo la kwanza unahitaji kujua ni kwamba taarifa juu ya hali yako ya VVU ni ya siri na ni juu yako, na wewe tu utakaeamua jinsi na wakati unapokuwa tayari kuwapa wengine habari.

Kuna faida nyingi zinazoweza kuwepo kwa kuwaambia wengine. Kuwaambia watu wengine hukusaidia kukubali kwamba unaishi na VVU. Kuwaambia wengine pia kuna maana kuwa una watu wa kukusaidia wakati unapoanza matibabu ya kutumia dawa.

Lakini ni muhimu pia kuwaambia watu ambao unawaamini. Na kuwaambia watu ambao unafikiri watasaidia. Fikiria mtu, kwa mfano rafiki wa karibu au mwana familia, ambaye unajua unaweza kuamini na hawezi kuto habari kwa wengine.

Ikiwezekana, unapaswa pia kumwambia mpenzi wako au washirika wako wa ngono una VVU, ili nao waweze kupima VVU pia. Ikiwa haiwezekani kufichua hali yako kwa mpenzi wako au washirika wako, una wajibu wa kuwalinda kutokana na maambukizi kwa kutumia kinga na njia nyingine za kuzuia VVU kama vile kutumia dawa mara kwa mara.

Ikiwa uko katika mahusiano ya muda mrefu, mara nyingi hupendeza kumwambia mpenzi wako kuwa una VVU kwa sababu usiofanya hivyo inaweza kupunguza kiwango cha uaminifu katika uhusiano na uwezekano wa mpenzi wako kuwa katika hatari ya kupata VVU.

Kumbuka una aina mbalimbali za kinga ya VVU ambazo wanaweza kutumia na washirika wako. Watu wengine wana uwezo wa kutumia kinga zaidi au wakati wote na hii inatoa kiwango cha juu cha ulinzi. Kwa wanandoa au washirika ambapo kutumia kondomu ni ngumu sana, machaguo tofauti yapo. Kwa mfano, kutumia dawa za kuongeza maisha ili virusi visiweze kuonekana  PrEP kwa watu wasio na VVU wanaweza kutumika pamoja kwa ajili ya ulinzi wa VVU.