Jambo bora kwa afya yako na ustawi wako ni kuacha matumizi ya vilevi kabisa lakini hii ni ngumu kwa wanaume wengi. Hata kama huwezi kuacha wote mara moja, bado kuna hatua ambazo unaweza kuchukua ili kupunguza hatari yako.
1. Jifunze kutambua ulevi na utegemezi wa madawa ya kulevya. Hatua ya kwanza ya kupata msaada kwa kutumia vilevi ni kutambua kwamba unaweza kuwa na utegemezi wa vilevi unavyotumia. Hizi ni ishara muhimu za kutazama:
- Unatamani madawa ya kulevya na daima unafikiria kupata zaidi
- Unakuwa na dalili za mwili kuchoka au kurukwa na akili unapoacha kuitumia
- Unaweza kuona kwamba kutumia madawa ya kulevya kumeanza kuingilia kati na maisha yako ya kazi au ya kibinafsi na kusababisha matatizo katika mahusiano yako
- Unaendelea kutumia madawa ya kulevya ingawa husababisha matokeo mabaya kwako
2. Ukijidunga madawa ya kulevya, tumia zana safi wakati unatumia na usishiriki sindano zilizotumiwa.
- VVU huambukizwa kwa urahisi sana unaposhiriki sindano kwa matumizi ya madawa ya kulevya. Hatari itakuwa chini ikiwa unatumia vifaa visafi wakati wa kujidunga sindano na ikiwa hautumii sindano za watu wengine
3. Pata zana za kuzuia VVU ambazo zinazokufaa.
- Weka kinga na mafuta-maji karibu yako utashiriki katika ngono wakati unatumia kilevi.
- Ikiwa huwezi kutumia kinga, ulizia mashirika ya mitaa karibu yako kuona kama dawa za kinga zinapatikana katika eneo lako.
- Angalia kama unaweza kupata dawa za kinga kabla hujahitaji. Kwa njia hii, ikiwa utagundua kuwa umeambukizwa, kupitia vifaa vya sindano au ngono bila kinga, basi unaweza kupata dawa za kinga haraka baada ya kuambukizwa.
4. Epuka kuchanganya vilevi
- Kuchanganya vilevi kuna athari mbaya na ya hatari. Kupunguza matumizi ya vilevi kuwa aina moja ya kilevi kila unapotumia hupunguza uwezekano wa madhara haya na VVU.
5. Punguza kuwa na watu au sehemu ambazo hukusababishia kutumia madawa ya kulevya.
- Unaweza kujaribu kuzuia au kupunguza kutembelea sehemu fulani au kwenye starehe na marafiki kama wana tabia za kukusababishia utumie vilevi.
6. Jiwekee lengo
- Ikiwa umeamua kubadilisha matumizi ya vilevi, basi weka lengo maalum ni mabadiliko gani unayoyataka. Hili litakupa mwongozo.
- Ni kawaida kuweka lengo la kubadilisha matumizi ya vilevi na kisha unashindwa. Mabadiliko ya matumizi ya vilevi ni magumu na inaweza kuchukua mara kufanikiwa. Kuwa na lengo kama mwongozo ni bora kwa sababu itakusaidia kurudi kwenye malengo ikiwa ulisahau mara ya kwanza.
Pata Msaada
- Kuacha matumizi ya vilevi au kubadilisha tabia yako ya matumizi ya vilevi ni ngumu sana na hupaswi kupitia hayo peke yako.
- Ongea na rafiki wa karibu ili aweze kujua hisia zako na anaweza kukusaidia katika mchakato huu.
- Unaweza pia kuwasiliana na shirika lililopo karibu yako kupata mwongozo wa ushauri nasaha au huduma nyingine.
- Inaweza kuwa rahisi kwako kuzungumza na mhudumu wa afya ikiwa unajisikia kama una tatizo na ulevi wa kisheria kama vile Pombe. Ikiwa unatumia kilevi kisicho cha kisheria, unaweza kujisikia aibu kuzungumza na mhudumu wa afya kuhusu hilo. Ikiwa ni hivyo, jaribu kuwasiliana na mashirika yaliyopo karibu nawe kuona kama wanaweza kukuelekeza kwa watoa huduma wa kirafiki