Afya yako ya akili inahusiana na jinsi unavyojihisi na akili yako inavyofanya kazi. Afya yako ya akili ni muhimu sana kwa sababu inaweza kuathiri afya yako ya kimwili na ustawi wako wote.
Wakati mtu ana shida ya afya ya akili, inamaanisha ustawi wao wa akili hauko sawa kama vile mwili wako unapoumia. Kuna sababu nyingi ambazo watu hupata masuala ya afya ya akili. Wanaume wengine huzaliwa katika hatari kubwa zaidi na wengine wana hatari baada ya kukabiliana na mambo kama msongo wa mawazo au shida.
Wakati mwingine matatizo ya afya ya akili yanaweza kuwa madogo na kuisha kwa urahisi. Nyakati nyingine yanaweza kuwa mabaya na kufanya iwe vigumu kwa watu kufanya kazi kama kawaida.
Wanaume wanaojamiiana na wanaume wengine wanaweza kupata matatizo ya afya ya akili kama huzuni na wasiwasi, sio kwa sababu ya wale wanaojamiiana nao lakini kwa sababu wanaweza kupata unyanyasaji, unyanyapaa, na ubaguzi.
Kuwa na uwezo wa kutambua ugonjwa wa akili ni muhimu kwa sababu wakati mwingine unaweza kukuongezea hatari ya kupata VVU kwa kuongeza matumizi ya vilevi au ya ngono hatari.
Pata maelezo zaidi kuhusu maswala mawili ya afya ya akili, Huzuni na Wasiwasi, na muhimu zaidi, wapi unaweza kupata msaada.