Wanaume Na Ngono - afya4men.info

Yale Wanaume Wanapaswa Kuyajua

Ngono ni hali ya kawaida ya maisha yetu. Wengi wetu hawathamini ngono bila kufikiria kuhusu umuhimu wake au bila kufikiria kuhusu maamuzi tunayoyafanya kuhusiana na ngono. Ngono ya kuwajibika inahusu kufanya maamuzi sahihi kwetu sisi na wenzi wetu kulingana na heshima ya pamoja, mawasiliano wazi na uaminifu na kulinda afya yetu na hata pia afya ya wenzi wetu.

Wale ambao wanaume wanafanya nao ngono

Baadhi yetu tuko katika mahusiano au tumeoa, wengine wako peke yao. Baadhi yetu tuna wenzetu  wa kingono kadhaa. Wanaume wengi wanafanya ngono tu na wanawake. Wengine wanafanya ngono na wanaume na wanawake. Baadhi wanafanya ngono tu na wanaume.

Wachache wetu tunajiita shoga (kuchu, msenge). Baadhi yetu tunajiita ‘bisexual’ kwa sababu tunavutiwa na wanawake na wanaume. Baadhi yetu pia tunajiita ‘Basha’.

Hatuwezi kuchagua kama tunavutiwa na wanawake ama wanaume au wote; hili silo jambo tunaloweza kuamua.

Hata hivyo, tunaweza kuchagua ni wanaume au wanawake wangapi tunaofanya ngono nao. Kufanya ngono na watu wachache hupunguza hatari yetu ya kupata virusi vya Ukimwi (HIV). Kufanya ngono na mtu mwenye umri wa chini ni kinyume cha sheria na ngono zote zinapaswa kuwa za kukubaliana.

Ngono ambazo wanaume hufanya

Kuna aina nyingi tofauti za ngono. Kubusu, ngono ya mdomo (kunyonya uume), ngono ya mkundu, ngono ya uke, ngono ya paja, na kupiga punyeto. Zote ni vitendo vya ngono tunavyoweza kuchagua kufanya na wenzi wetu. Wengine wanapenda kufanya ngono na watu wengi kwa mara moja. Baadhi ya vitendo hivi vina hatari zaidi ya kupata vijidudu vya HIV zaidi ya vingine. Kwa mfano, ngono ya mkundu bila kondomu na mafuta ya kulainisha ya maji ina hatari ya juu zaidi ya kupata virusi vya HIV au kuwaambukiza wengine. Tunaweza pia kuchagua kumwamini mpenzi wakati anapotueleza kuwa hana HIV, au kuwatendea wapenzi wetu wote kama wanaweza kutuambukiza.

Wakati wanaume wanapofanya ngono

Tunaweza kufanya ngono wakati tunahisi tunaweza kujidhibiti au tunaweza kufanya ngono wakati tumekuwa tukilewa au kutumia dawa za kulevya na huenda tusiweze kufanya maamuzi ya busara. Tukifikiria kwamba tutafanya ngono na wanaume wenzetu au wanawake, tunapaswa kuhakikisha tunaweza kupata kondomu na mafuta ya kulainisha ya maji.